Mvua ya Elnino yatarajiwa kuanza wiki hii

0
Oplus_131072

Na Felistars Kahungu

Kenya imeingia rasmi katika msimu wa mvua wa Oktoba-Desemba, huku Huduma ya Hali ya Hewa ya Kenya ikionya kuhusu hali ya mvua kupita kawaida katika sehemu kadhaa za nchi na kutoa tarehe maalum za kaunti za kuanza kwa mvua.

Kaimu mkuu wa Mamlaka ya Huduma za Hali ya Hewa ya Kenya Edward Muriuki amesema mvua imeanza katika sehemu za kaunti ishrini na nne ikiwa ni pamoja na Pwani, magharibi mwa Kenya na Bonde la Ufa, na iitaendelea kuenea hadi maeneo mengine.Hata hivyo amesema kaunti  ambazo zimebaki zitapata mvua wiki hii au wiki inayofuata, huku Turkana na Samburu zikitarajiwa kuwa za mwisho kupata mvua hiyo katika wiki ya tatu au ya nne ya Oktoba.

Muriuki amewasihi wakulima kutegemea utabiri wa kina unaotolewa na maafisa wa hali ya hewa wa kaunti kwa sababu mwanzo na nguvu ya mvua itatofautiana katika maeneo mbalimbali.

Hata hivyo Mvua tayari imeanza katika maeneo ya Nandi, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Siaya, Busia, Baringo, Nakuru, Trans Nzoia, Uasin Gishu, Elgeyo Marakwet, Pokot Magharibi, Kisii, Nyamira, Kericho, Bomet, Kisumu, Homa Bay, Migori na Narok.Hata hivyo,wataalamu wa hali ya hewa  imeonya kwamba mvua mingi inaweza kusababisha maji kujaa, magonjwa ya mazao, kuvurugika kwa shughuli za kilimo na ugumu wa kusafirisha mazao ya kilimo.

Shirika hilo linatarajia mvua kubwa hasa katika sehemu za Pwani na kaskazini mashariki mwa Kenya, ikiwa ni pamoja na Kwale, Mombasa, Kilifi, Lamu na Mandera, pamoja na sehemu za Taita Taveta, Tana River, Garissa na Wajir.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *