MWANAMUME ALIYEMSHAMBULIA MWANAMKE KUZUILIWA

Picha kwa hisani ya Citizen Digital
Imeandikwa na Felistars Kahungu
Mwanamume aliyenaswa kwenye video akimshambulia mwanamke huko Kamakis, Kaunti Ndogo ya Ruiru, amezuiliwa kwa siku 14 ili kuruhusu polisi kukamilisha uchunguzi wao.
Isaac Ochalo, ambaye alikamatwa siku moja kabla ya kufikishwa mahakamani, ameshtakiwa kwa shambulio lililosababisha madhara ya mwili.
Hata hivyo alikana mashtaka hayo
.Mahakama Kuu Yafutilia Mbali Ombi la Kufungia KUSCCOKamanda wa Polisi wa Ruiru Charles Kibathi alisema mahakama iliwapa makachero siku 14 kumzuilia mshukiwa kwa uchunguzi zaidi na mahojiano.
Atazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Gatong’ora kwa sasa.Kulingana na ripoti ya polisi, Teresia Wambui Wairimu, mkazi wa Thika Town, alishambuliwa Jumapili jioni alipokuwa akimtembelea binamu yake katika eneo la Kamakis huko Ruiru.
Wairimu aliwaambia polisi kwamba alifika nyumbani kwa binamu yake yapata saa kumi na mbili jioni, wakati mume wa binamu yake, aliyetambuliwa kama Isaac Gatuthu Ocharo, alipomshambulia.Maafisa wa polisi waliotembelea eneo la tukio waligundua kuwa mshukiwa alikuwa akigombana na mkewe wakati Wairimu alipoingilia kati.Inadaiwa alimgeukia na kumshambulia kimwili.
Wairimu baadaye alipelekwa katika Hospitali ya Ruiru Level 4 kwa ajili ya uchunguzi wa kimatibabu. Hali yake haijawekwa wazi.Tukio hilo lilinaswa kwenye video, jambo lililosababisha hatua ya polisi iliyosababisha mshukiwa kukamatwa.inayovuma sasa