Wanyang’anyi wawili wa simu wakamatwa

Na Felistars Kahungu
Washukiwa wawili waliopora simu mbili za mkononi kutoka kwa mwananchi wamekamatwa katika msako mkali katika maeneo ya Clay City, Sunton na Hunters, Kasarani.
Washukiwa hao wamekamatwa Jumapili baada ya kujaribu kukwepa kukamatwa, na kuzua shaka zaidi miongoni mwa maafisa wa polisi.
Kulingana na huduma ya kitaifa ya polisi Wawili hao walijaribu kukwepa kukamatwa, na kusababisha kufukuzwa haraka na maafisa, ambao waliwakamataHata hivyo Washukiwa hao wako kizuizini mwa polisi wakisubiri kufikishwa mahakamani, huku silaha hizo ghafi zikishikiliwa kama ushahidi.