Marekani yamkamata mwanamke anayetuhumiwa kuipeleleza familia ya kiongozi wa Taiwan

0
Picha Kwa hisani ya Citizen Digital

Na Felistars Kahungu

Mwanamke mwenye umri wa miaka thelathini na nne, Wanying Zhang, amekamatwa nchini Marekani kwa tuhuma za kuipeleleza China dhidi ya familia ya Rais wa Taiwan, Lai Ching-te.

Zhang amekamatwa na FBI katika uwanja wa ndege wa Los Angeles alipokuwa akijaribu kusafiri kwenda China. Amehusishwa na tuhuma za kuwa wakala asiyesajiliwa wa China na kufuatilia mwana wa Lai pamoja na familia yake.

Inadaiwa kuwa Zhang amekuwa akirekodi video za nyumba na magari yao, pamoja na kutuma picha, video na taarifa za nambari za usajili kwa maafisa wa China.

Aidha, amedaiwa kutumia mbinu za kibiashara ili kuepuka kugunduliwa.Ofisi ya Rais wa Taiwan imekemea vikali kitendo hicho, ikikitaja kuwa ni aina ya “ukandamizaji wa kimataifa”, huku ikiishukuru Marekani kwa ulinzi na msaada wake.

Hata hivyo China imeendelea kuidai Taiwan kuwa sehemu ya eneo lake, huku Taiwan ikiwa imeonya raia wake kuhusu hatari zinazoongezeka za usalama nchini China na maeneo mengine.Zhang, ambaye amekuwa akiishi Irvine, California, anatarajiwa kufikishwa katika mahakama ya shirikisho nchini Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *