Orodha ya matakwa ya Mudavadi kwa  mwaka wa elf u mbili ishirini na saba

0
Picha kwa hisani ya The Star

Na Felistars Kahungu

Waziri Mkuu Musalia Mudavadi ametoa wito wa kuwepo kwa taasisi imara na ulinzi wa uhuru wa tume ya uchaguzi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Mudavadi amesema Kenya lazima iimarishe taasisi zake ili kulinda maadili ya kidemokrasia, kukuza utulivu wa kitaifa na kuhakikisha mchakato wa uchaguzi unaoaminika.

Hata hivyo Mudavadi amesema nchi lazima ijifunze kutokana na uzoefu wa muda mrefu wa ujenzi wa taifa wa China huku ikiendeleza taasisi zake.Amechagua Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), akisema uhuru wake lazima uimarishwe na kulindwa ili kulinda uadilifu wa uchaguzi.

Mudavadi amehusisha hitaji la taasisi imara na ajenda ya maendeleo ya nchi, akitaja mfumo mpya wa maendeleo ambao timu ya Rais William Ruto inaushinikiza huku Dira ya mwaka wa elfu mbili na thelathini ikikaribia kukamilika.

Mudavadi pia aliangazia uhusiano unaokua wa kisiasa na kiuchumi kati ya Kenya na China.Hata hivyo Amseema ushirikiano huo umesababisha makubaliano yanayohusu fedha, utengenezaji na uongezaji thamani, miundombinu, afya, utalii, utamaduni na elimu.Mudavadi alinukuu hasa Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa Maendeleo kati ya China na Afrika (CADEPA), ambapo Kenya na China zimeitia saini Mkataba wa Mavuno ya Mapema mwezi Machi mwaka huu.

Mpangilio huo, ambao ulianza kutumika Mei, unaruhusu mauzo ya nje ya Kenya kwenda China kuingia sokoni bila ushuru.Mudavadi amesema makubaliano hayo tayari yanaunga mkono ukuaji wa mauzo ya nje ya bidhaa kama vile kahawa, parachichi na chai.

Fauka ya hayo amesema Kenya iko tayari kuanza mazungumzo ya kina na China kuhusu nyanja zote za CADEPA, akisema kwamba hii itafungua fursa za uwekezaji na kuboresha uwezo wa Kenya kushindana katika soko la China.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *