Wawili wakamatwa kwa kutengeneza juisi bandia huko Kabete

0
Oplus_131072

Picha kwa hisani ya Citizen Digital

Na Felistars Kahungu

Makachero kutoka kituo cha polisi cha Kabete wamewakamata washukiwa wawili wanaodaiwa  kutengeneza juisi bandia nyumbani kwao Muthua, Kabete.

Washukiwa hao wawili, wametambuliwa kama Alex Mwaruta na James Munala Inyangala, wamekamatwa  wakitengeneza juisi bandia kufuatia filimbi kutoka kwa mwananchi.

Hata hivyo Wakati wa msako huo, wapelelezi wamepata takriban chupa elfu moja na mia nne (1,400 ) ambazo zimejaa  zenye ujazo wa mililita 200 na mililita 300 za juisi bandia, katoni hamsini na sita za chupa tupu, pakiti tano za vifuniko vya chupa, ngoma mbili za bluu na beseni tatu za rangi mbalimbali.

Fauka ya hayo wamepata gundi ya ofisini, stempu za mpira na wino, stika mbalimbali, cheti kilichopitwa na wakati kinachoidhinisha matumizi ya Alama ya Usanifishaji kwa chapa maarufu ya juisi na vitu mbalimbali vya unga na visivyo na rangi vilivyopakiwa kwenye mifuko ya nailoni katika sehemu za gramu hamsini na katika chupa za mililita mia mbili na mililita mia tatuVitu hivyo vimehidhiwa kama vielelezo baada ya kushughulikiwa na wapelelezi kutoka Upelelezi wa Eneo la Uhalifu (CSI).

Na kwa sasa Washukiwa sasa wako chini ya ulinzi wa polisi.

L

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *