Rais Ruto aomboleza kifo cha Wicknell Chivayo aliyefariki katika ajali ya helikopta

Na Felistars Kahungu
Rais William Ruto ameomboleza kifo cha kusikitisha cha rafiki yake mpendwa, mfanyabiashara wa Zimbabwe Wicknell Chivayo, ambaye amefariki katika ajali ya helikopta nchini Zimbabwe.
Chivayo na mkewe, Lucy Muteke, ni miongoni mwa watu sita waliouawa baada ya helikopta yao kuanguka katika eneo la Marondera Vijijini, Rais Ruto na Chivayo walikuwa wameanzisha urafiki ambao mara nyingi ulishangaza taifa zima,.
Ameeleza masikitiko yake kufuatia kifo cha rafiki yake Wicknell Chivayo, mkewe Lucy Muteke na watu wengine waliopoteza maisha katika ajali ya helikopta nchini Zimbabwe.
Amemtaja Chivayo kama rafiki mpendwa aliyekuwa na uchangamfu, nguvu na imani kubwa katika maendeleo ya Afrika. Aidha, ametuma rambirambi kwa familia za waliofiwa huku nayeRais Emmerson Mnangagwa na wananchi wa Zimbabwe, akiwaombea marehemu wote wapate mapumziko ya milele.