Rais Ruto awahakikishia wakazi wa Lamu masuala ya ardhi yatashughulikiwa kisheria

0
Picha kwa hisani ya Citizen Digital

Na Felistars Kahungu

Rais William Ruto amewahakikishia wakazi wa Lamu kwamba wasiwasi kuhusu kipande cha ardhi chenye ukubwa wa zaidi ya ekari efu saba( 7,000 )ambapo Kiwanda cha Kusafisha Mafuta cha Dangote East Africa kitajengwa utashughulikiwa kwa haki na kwa mujibu wa sheria.

Ruto, ambaye ameongoza sherehe ya uzinduzi wa mradi huo wa  trilioni mbili nukta mbili( Ksh.2.2 trilioni )pamoja na bilionea wa Nigeria Aliko Dangote, amesema kiwanda hicho kitakamilika ndani ya miaka mitatu na kuunda zaidi ya ajira  elfu sitini 60,000

Hata hivyo Uvumbuzi huo umeanzishwa  baada ya siku za maandamano na maombi kutoka kwa wakazi kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kusafishia mafuta na fidia ya ardhi.

Fauka ya hayo Dangote ameahidi kurejea nchini na kuanza ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta ndani ya miezi arobaini, huku akiahidi kuanzisha shule ya mafunzo huko Lamu ambayo imepangwa kuwafunza watu elfu moja wenye diploma au shahada za uhandisi.Hata hivyo, Rais William Ruto ameonya kuwa Wakenya wamekuwa wakifuatilia ratiba hiyo na wamesubiri ahadi hiyo itimizwe.

Aidha, amewahakikishia wakazi wa Lamu kuwa masuala ya ardhi na fidia yameshughulikiwa kwa mujibu wa sheria na kwa haki.Ruto amesema kuwa mradi huo umetoa fursa za ajira na biashara kwa wakazi wa Lamu, huku Dangote amesisitiza kuwa amekuwa tayari kukabiliana na changamoto za kisheria na upinzani dhidi ya mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *